IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Masharti ya qiraa katika Mashindano ya Kimataifa ya  Qur'ani ya Meshkat

19:34 - January 14, 2024
Habari ID: 3478196
IQNA - Waandaaji wa Awamu ya Tatu ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Meshkat wametangaza kanuni na vigezo vya kuwasilisha visomo vya qiraa ya Qur'ani iliyorekodiwa.

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Meshkat ni tukio la mtandaoni ambalo huandaliwa na Taasisi ya Qur'ani ya Meshkat kwa ushirikiano na Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Imam Ridha AS (Astan Quds Razavi)

Yakiwa yamepangwa kufanyika Februari, mashindano hayo yamepangwa kufanyika katika kategoria za usomaji wa Qur'ani wa mbinu ya Taqlid yaani kuiga kwa wanaume na kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa wanaume na wanawake.

Inalenga kukuza Qur'ani Tukufu, kuimarisha umoja katika Umma wa Kiislamu na kuwaenzi wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani wa ulimwengu wa Kiislamu.

Wale ambao wako tayari kushiriki katika kategoria ya qiraa wanahitaji kutuma video iliyorekodiwa ya usomaji wao wakiiga mojawapo ya visomo vinne vilivyochaguliwa na Maqarii au wasomaji maarufu ambao ni  Sheikh Mohamed Siddiq El-Minshawi, Sheikh Abdul Basit Abdul Samad, Sheikh Shahat Muhammad Anwar, na Sheikh Mustafa Ismail.

Kwa mujibu wa sekretarieti ya shindano hilo, tarehe ya mwisho ya kuwasilisha visomo ni Februari 19.

Usomaji wao lazima usiwe zaidi ya dakika 6 na faili lazima iwe na jina la kwanza, jina la ukoo, umri, na mahali pa kuishi.

Usomaji lazima urekodiwe kwa mlalo na kamera moja pekee, bila madoido ya sauti, bila kuhariri, na bila kusimama au kusitisha.

Video zilizowasilishwa zitatolewa mtandaoni baada ya kumalizika kwa shindano.

Hapo awali, mkurugenzi wa Taasisi ya Meshkat Hujjatul Islam Mojtaba Mohammadi alisema tarehe ya mwisho ya kujiandikisha ni Januari 20, na wanaotaka kushiriki wanaweza kutuma maombi kupitia tovuti ya taasisi hiyo.

Alibainisha kuwa washindi wa kila kipengele watapata zawadi ya fedha taslimu karibu dola 2,000, huku washindi wa pili na washindi wa tatu watapata karibu dola 1,600 na dola 1,400 mtawalia.

Toleo la awali la shindano hilo lililofanyika mwaka jana, lilivutia washiriki zaidi ya 1,000 kutoka nchi 73, 153 kati yao walifanikiwa kuingia hatua ya fainali.

3486798

captcha